149 Uisikie sauti yangu sawasawa na fadhili zako,Ee BWANA, unihuishe sawasawa na hukumu yako.
150 Wanakaribia wanaonifuatia kwa chuki,Wamekwenda mbali na sheria yako.
151 Ee BWANA, Wewe U karibu,Na maagizo yako yote ni kweli.
152 Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako,Ya kuwa umeziweka zikae milele.
153 Uyaangalie mateso yangu, uniokoe,Maana sikuisahau sheria yako.
154 Unitetee na kunikomboa,Unihuishe sawasawa na ahadi yako.
155 Wokovu u mbali na wasio haki,Kwa maana hawajifunzi amri zako.