155 Wokovu u mbali na wasio haki,Kwa maana hawajifunzi amri zako.
156 Ee BWANA, rehema zako ni nyingi,Unihuishe sawasawa na hukumu zako.
157 Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi,Lakini sikujiepusha na shuhuda zako.
158 Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa,Kwa sababu hawakulitii neno lako.
159 Uangalie niyapendavyo mausia yako,Ee BWANA, unihuishe sawasawa na fadhili zako.
160 Jumla ya neno lako ni kweli,Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.
161 Wakuu wameniudhi bure,Ila moyo wangu unayahofia maneno yako.