160 Jumla ya neno lako ni kweli,Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.
161 Wakuu wameniudhi bure,Ila moyo wangu unayahofia maneno yako.
162 Naifurahia ahadi yako,Kama apataye mateka mengi.
163 Nimeuchukia uongo, umenikirihi,Sheria yako nimeipenda.
164 Mara saba kila siku nakusifu,Kwa sababu ya hukumu za haki yako.
165 Wana amani nyingi waipendao sheria yako,Wala hawana la kuwakwaza.
166 Ee BWANA, nimeungojea wokovu wako,Na maagizo yako nimeyatenda.