167 Nafsi yangu imezishika shuhuda zako,Nami nazipenda mno.
168 Nimeyashika mausia yako na shuhuda zako,Maana njia zangu zote zi mbele zako.
169 Ee BWANA, kilio changu na kikukaribie,Unifahamishe sawasawa na neno lako.
170 Dua yangu na ifike mbele zako,Uniponye sawasawa na ahadi yako.
171 Midomo yangu na itoe sifa,Kwa kuwa unanifundisha mausia yako.
172 Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako,Maana maagizo yako yote ni ya haki.
173 Mkono wako na uwe tayari kunisaidia,Maana nimeyachagua mausia yako.