171 Midomo yangu na itoe sifa,Kwa kuwa unanifundisha mausia yako.
172 Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako,Maana maagizo yako yote ni ya haki.
173 Mkono wako na uwe tayari kunisaidia,Maana nimeyachagua mausia yako.
174 Ee BWANA, nimeutamani wokovu wako,Na sheria yako ndiyo furaha yangu.
175 Nafsi yangu na iishi, ipate kukusifu,Na hukumu zako zinisaidie.