18 Unifumbue macho yangu niyatazameMaajabu yatokayo katika sheria yako.
19 Mimi ni mgeni katika nchi,Usinifiche maagizo yako.
20 Roho yangu imepondeka kwa kutamaniHukumu zako kila wakati.
21 Umewakemea wenye kiburi,Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo yako.
22 Uniondolee laumu na dharau,Kwa maana nimezishika shuhuda zako.
23 Wakuu nao waliketi wakaninena,Lakini mtumishi wako atazitafakari amri zako.
24 Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu,Na washauri wangu.