25 Nafsi yangu imeambatana na mavumbi,Unihuishe sawasawa na neno lako.
26 Nalizisimulia njia zangu ukanijibu,Unifundishe amri zako.
27 Unifahamishe njia ya mausia yako,Nami nitayatafakari maajabu yako.
28 Nafsi yangu imeyeyuka kwa uzito,Unitie nguvu sawasawa na neno lako.
29 Uniondolee njia ya uongo,Unineemeshe kwa sheria yako.
30 Nimeichagua njia ya uaminifu,Na kuziweka hukumu zako mbele yangu.
31 Nimeambatana na shuhuda zako,Ee BWANA, usiniaibishe.