32 Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako,Utakaponikunjua moyo wangu.
33 Ee BWANA, unifundishe njia ya amri zako,Nami nitaishika hata mwisho.
34 Unifahamishe nami nitaishika sheria yako,Naam, nitaitii kwa moyo wangu wote.
35 Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako,Kwa maana nimependezwa nayo.
36 Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako,Wala usiielekee tamaa.
37 Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa,Unihuishe katika njia yako.
38 Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako,Inayohusu kicho chako.