36 Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako,Wala usiielekee tamaa.
37 Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa,Unihuishe katika njia yako.
38 Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako,Inayohusu kicho chako.
39 Uniondolee laumu niiogopayo,Maana hukumu zako ni njema.
40 Tazama, nimeyatamani mausia yako,Unihuishe kwa haki yako.
41 Ee BWANA, fadhili zako zinifikie na mimi,Naam, wokovu wako sawasawa na ahadi yako.
42 Nami nitamjibu neno anilaumuye,Kwa maana nalitumainia neno lako.