47 Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako,Ambayo nimeyapenda.
48 Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda,Nami nitazitafakari amri zako.
49 Likumbuke neno ulilomwambia mtumishi wako,Kwa sababu umenitumainisha.
50 Hii ndiyo faraja yangu katika taabu yangu,Ya kwamba ahadi yako imenihuisha.
51 Wenye kiburi wamenidharau mno,Sikujiepusha na sheria zako.
52 Nimezikumbuka hukumu zako za kale,Ee BWANA, nikajifariji.
53 Ghadhabu imenishika kwa sababu ya wasio haki,Waiachao sheria yako.