5 Ningependa njia zangu ziwe thabiti,Nizitii amri zako.
6 Ndipo mimi sitaaibika,Nikiyaangalia maagizo yako yote.
7 Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo,Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako
8 Nitazitii amri zako,Usiniache kabisa
9 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?Kwa kutii, akilifuata neno lako.
10 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta,Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,Nisije nikakutenda dhambi.