51 Wenye kiburi wamenidharau mno,Sikujiepusha na sheria zako.
52 Nimezikumbuka hukumu zako za kale,Ee BWANA, nikajifariji.
53 Ghadhabu imenishika kwa sababu ya wasio haki,Waiachao sheria yako.
54 Amri zako zimekuwa nyimbo zangu,Katika nyumba ya ugeni wangu.
55 Wakati wa usiku nimelikumbuka jina lako,Ee BWANA, nikaitii sheria yako.
56 Hayo ndiyo niliyokuwa nayo,Kwa sababu nimeyashika mausia yako.
57 BWANA ndiye aliye fungu langu,Nimesema kwamba nitayatii maneno yake.