6 Ndipo mimi sitaaibika,Nikiyaangalia maagizo yako yote.
7 Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo,Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako
8 Nitazitii amri zako,Usiniache kabisa
9 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?Kwa kutii, akilifuata neno lako.
10 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta,Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,Nisije nikakutenda dhambi.
12 Ee BWANA, umehimidiwa,Unifundishe amri zako.