64 BWANA, dunia imejaa fadhili zako,Unifundishe amri zako.
65 Umemtendea mema mtumishi wako,Ee BWANA, sawasawa na neno lako.
66 Unifundishe akili na maarifa,Maana nimeyaamini maagizo yako.
67 Kabla sijateswa mimi nalipotea,Lakini sasa nimelitii neno lako.
68 Wewe U mwema na mtenda mema,Unifundishe amri zako.
69 Wenye kiburi wamenizulia uongo,Kwa moyo wangu wote nitayashika mausia yako.
70 Mioyo yao imenenepa kama shahamu,Mimi nimeifurahia sheria yako.