70 Mioyo yao imenenepa kama shahamu,Mimi nimeifurahia sheria yako.
71 Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa,Nipate kujifunza amri zako.
72 Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu,Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
73 Mikono yako ilinifanya ikanitengeneza,Unifahamishe nikajifunze maagizo yako.
74 Wakuchao na wanione na kufurahi,Kwa sababu nimelingojea neno lako.
75 Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki,Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa.
76 Nakuomba, fadhili zako ziwe faraja kwangu,Sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.