78 Wenye kiburi waaibike, maana wamenidhulumu kwa uongo,Mimi nitayatafakari mausia yako.
79 Wakuchao na wanirudie,Nao watazijua shuhuda zako.
80 Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri zako,Nisije mimi nikaaibika.
81 Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako,Nimelingojea neno lako.
82 Macho yangu yamefifia kwa kuitazamia ahadi yako,Nisemapo, Lini utakaponifariji?
83 Maana nimekuwa kama kiriba katika moshi,Sikuzisahau amri zako.
84 Siku za mtumishi wako ni ngapi,Lini utakapowahukumu wale wanaonifuatia?