83 Maana nimekuwa kama kiriba katika moshi,Sikuzisahau amri zako.
84 Siku za mtumishi wako ni ngapi,Lini utakapowahukumu wale wanaonifuatia?
85 Wenye kiburi wamenichimbia mashimo,Ambao hawaifuati sheria yako.
86 Maagizo yako yote ni amini,Wananifuatia bure, unisaidie.
87 Walikuwa karibu na kunikomesha katika nchi,Lakini sikuyaacha mausia yako.
88 Unihuishe kwa fadhili zako,Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.
89 Ee BWANA, neno lako lasimamaImara mbinguni hata milele.