85 Wenye kiburi wamenichimbia mashimo,Ambao hawaifuati sheria yako.
86 Maagizo yako yote ni amini,Wananifuatia bure, unisaidie.
87 Walikuwa karibu na kunikomesha katika nchi,Lakini sikuyaacha mausia yako.
88 Unihuishe kwa fadhili zako,Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.
89 Ee BWANA, neno lako lasimamaImara mbinguni hata milele.
90 Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi,Umeiweka nchi, nayo inakaa.
91 Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo,Maana vitu vyote ni watumishi wako.