90 Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi,Umeiweka nchi, nayo inakaa.
91 Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo,Maana vitu vyote ni watumishi wako.
92 Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu,Hapo ningalipotea katika taabu zangu.
93 Hata milele sitayasahau maagizo yako,Maana kwa hayo umenihuisha.
94 Mimi ni wako, uniokoe,Kwa maana nimejifunza mausia yako.
95 Wasio haki wameniotea ili kunipoteza,Nitazitafakari shuhuda zako.
96 Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho,Bali agizo lako ni pana mno.