1 Nitayainua macho yangu niitazame milima,Msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu u katika BWANA,Aliyezifanya mbingu na nchi.
3 Asiuache mguu wako usogezwe;Asisinzie akulindaye;
4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi,Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 BWANA ndiye mlinzi wako;BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.