2 Miguu yetu imesimamaNdani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
3 Ee Yerusalemu uliyejengwaKama mji ulioshikamana,
4 Huko ndiko walikopanda kabila,Kabila za BWANA;Ushuhuda kwa Israeli,Walishukuru jina la BWANA.
5 Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.
6 Utakieni Yerusalemu amani;Na wafanikiwe wakupendao;
7 Amani na ikae ndani ya kuta zako,Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zanguNiseme sasa, Amani ikae nawe.