1 Nimekuinulia macho yangu,Wewe uketiye mbinguni.
2 Kama vile macho ya watumishiKwa mkono wa bwana zaoKama macho ya mjakaziKwa mkono wa bibi yake;Hivyo macho yetu humwelekea BWANA, Mungu wetu,Hata atakapoturehemu.
3 Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu sisi,Kwa maana tumeshiba dharau.