1 Haleluya.Lisifuni jina la BWANA,Enyi watumishi wa BWANA, sifuni.
2 Ninyi msimamao nyumbani mwa BWANA,Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu.
3 Msifuni BWANA kwa kuwa BWANA ni mwema,Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza.
4 Kwa sababu BWANA amejichagulia Yakobo,Na Israeli, wawe watu wake hasa.
5 Maana najua mimi ya kuwa BWANA ni mkuu,Na Bwana wetu yu juu ya miungu yote.
6 BWANA amefanya kila lililompendeza,Katika mbingu na katika nchi,Katika bahari na katika vilindi vyote.