11 Sihoni, mfalme wa Waamori,Na Ogu, mfalme wa Bashani,Na falme zote za Kanaani.
12 Akaitoa nchi yao iwe urithi,Urithi wa Israeli watu wake.
13 Ee BWANA, jina lako ni la milele,BWANA, kumbukumbu lako vizazi hata vizazi.
14 Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake,Atawahurumia watumishi wake.
15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,Kazi ya mikono ya wanadamu.
16 Zina vinywa lakini hazisemi,Zina macho lakini hazioni,
17 Zina masikio lakini hazisikii,Wala hamna pumzi vinywani mwake.