15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,Kazi ya mikono ya wanadamu.
16 Zina vinywa lakini hazisemi,Zina macho lakini hazioni,
17 Zina masikio lakini hazisikii,Wala hamna pumzi vinywani mwake.
18 Wazifanyao watafanana nazo,Na kila mmoja anayezitumainia.
19 Enyi mlango wa Israeli, mhimidini BWANA;Enyi mlango wa Haruni, mhimidini BWANA;
20 Enyi mlango wa Lawi, mhimidini BWANA;Ninyi mnaomcha BWANA, mhimidini BWANA.