17 Zina masikio lakini hazisikii,Wala hamna pumzi vinywani mwake.
18 Wazifanyao watafanana nazo,Na kila mmoja anayezitumainia.
19 Enyi mlango wa Israeli, mhimidini BWANA;Enyi mlango wa Haruni, mhimidini BWANA;
20 Enyi mlango wa Lawi, mhimidini BWANA;Ninyi mnaomcha BWANA, mhimidini BWANA.