6 BWANA amefanya kila lililompendeza,Katika mbingu na katika nchi,Katika bahari na katika vilindi vyote.
7 Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi;Huifanyia mvua umeme;Hutoa upepo katika hazina zake.
8 Aliwapiga wazaliwa wa kwanza wa Misri,Wa wanadamu na wa wanyama.
9 Alipeleka ishara na maajabu kati yako, Ee Misri,Juu ya Farao na watumishi wake wote.
10 Aliwapiga mataifa mengi,Akawaua wafalme wenye nguvu;
11 Sihoni, mfalme wa Waamori,Na Ogu, mfalme wa Bashani,Na falme zote za Kanaani.
12 Akaitoa nchi yao iwe urithi,Urithi wa Israeli watu wake.