1 Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi,Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.
2 Katika miti iliyo katikati yakeTulivitundika vinubi vyetu.
3 Maana huko waliotuchukua matekaWalitaka tuwaimbie;Na waliotuonea walitaka furaha;Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.
4 Tuuimbeje wimbo wa BWANAKatika nchi ya ugeni?