3 Siku ile niliyokuita uliniitikia,Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
4 Ee BWANA, wafalme wote wa dunia watakushukuru,Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.
5 Naam, wataziimba njia za BWANA,Kwa maana utukufu wa BWANA ni mkuu.
6 Ingawa BWANA yuko juu, amwona mnyenyekevu,Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
7 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha,Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu,Na mkono wako wa kuume utaniokoa.