1 Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.
2 Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,Umeelewa na njia zangu zote.
4 Maana hamna neno ulimini mwanguUsilolijua kabisa, BWANA.