14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwaKwa jinsi ya ajabu ya kutisha.Matendo yako ni ya ajabu,Na nafsi yangu yajua sana,
15 Mifupa yangu haikusitirika kwako,Nilipoumbwa kwa siri,Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika;Chuoni mwako ziliandikwa zote pia,Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
17 Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu;Jinsi ilivyo kubwa jumla yake!
18 Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga;Niamkapo nikali pamoja nawe.
19 Ee Mungu, laiti ungewafisha waovu!Enyi watu wa damu, ondokeni kwangu;
20 Kwa maana wakuasi kwa ubaya,Adui zako wakutaja jina lako bure.