17 Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu;Jinsi ilivyo kubwa jumla yake!
18 Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga;Niamkapo nikali pamoja nawe.
19 Ee Mungu, laiti ungewafisha waovu!Enyi watu wa damu, ondokeni kwangu;
20 Kwa maana wakuasi kwa ubaya,Adui zako wakutaja jina lako bure.
21 Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia?Nisikirihike nao wakuasio?
22 Nawachukia kwa ukomo wa chuki,Wamekuwa adui kwangu.
23 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu,Unijaribu, uyajue mawazo yangu;