5 Umenizingira nyuma na mbele,Ukaniwekea mkono wako.
6 Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi,Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.
7 Niende wapi nijiepushe na roho yako?Niende wapi niukimbie uso wako?
8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi,Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 Huko nako mkono wako utaniongoza,Na mkono wako wa kuume utanishika.
11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika,Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;