8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi,Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 Huko nako mkono wako utaniongoza,Na mkono wako wa kuume utanishika.
11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika,Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;
12 Giza nalo halikufichi kitu,Bali usiku huangaza kama mchana;Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwaKwa jinsi ya ajabu ya kutisha.Matendo yako ni ya ajabu,Na nafsi yangu yajua sana,