1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo,Hakuna atendaye mema.
2 Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu,Aone kama yuko mtu mwenye akili,Amtafutaye Mungu.
3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja,Hakuna atendaye mema,La! Hata mmoja.
4 Je! Wote wafanyao maovu hawajui?Walao watu wangu kama walavyo mkate,Hawamwiti BWANA.
5 Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi,Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.
6 Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge,Bali BWANA ndiye aliye kimbilio lake.