1 Ee BWANA, uniokoe na mtu mbaya,Unihifadhi na mtu wa jeuri.
2 Waliowaza mabaya mioyoni mwao,Kila siku huondokesha vita.
3 Wamenoa ndimi zao kama nyoka,Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
4 Ee BWANA, unilinde na mikono ya mtu asiye haki;Unihifadhi na mtu wa jeuri;Waliowaza kuzipotosha hatua zangu.