2 Waliowaza mabaya mioyoni mwao,Kila siku huondokesha vita.
3 Wamenoa ndimi zao kama nyoka,Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
4 Ee BWANA, unilinde na mikono ya mtu asiye haki;Unihifadhi na mtu wa jeuri;Waliowaza kuzipotosha hatua zangu.
5 Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba;Wametandika wavu kando ya njia;Wameniwekea matanzi.
6 Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu;Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu.
7 Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu,Umenifunika kichwa changu siku ya vita.
8 Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake,Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua.