6 Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu;Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu.
7 Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu,Umenifunika kichwa changu siku ya vita.
8 Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake,Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua.
9 Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka,Madhara ya midomo yao yawafunike.
10 Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni,Na katika mashimo, wasipate kusimama tena.
11 Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi,Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza.
12 Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu,Na wahitaji haki yao.