8 Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi,Kwa maana nimekutumaini Wewe.Unijulishe njia nitakayoiendea,Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.
9 Ee BWANA, uniponye na adui zangu;Nimekukimbilia Wewe, unifiche.
10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako,Kwa maana ndiwe Mungu wangu;Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa,
11 Ee BWANA, unihuishe kwa ajili ya jina lako,Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;