10 Awapaye wafalme wokovu,Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.
11 Uniponye, unitoe,Katika mkono wa wageni.Vinywa vyao vyasema visivyofaa,Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
12 Wana wetu na wawe kama micheWaliokua ujanani.Binti zetu kama nguzo za pembeniZilizonakishwa kwa kupamba hekalu.
13 Ghala zetu na zijaeZenye akiba za jinsi zote.Kondoo zetu na wazaeElfu na makumi elfu mashambani mwetu.
14 Ng’ombe zetu na wachukue mizigo,Kusiwe na kushambuliwa.Wala kusiwe na kuhamishwa,Wala malalamiko katika njia zetu.