1 Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza,Nitalihimidi jina lako milele na milele.
2 Kila siku nitakuhimidi,Nitalisifu jina lako milele na milele.
3 BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,Wala ukuu wake hautambulikani.
4 Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako,Kitayatangaza matendo yako makuu.
5 Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako,Na matendo yako yote ya ajabu.
6 Watu watayataja matendo yako ya kutisha,Nami nitausimulia ukuu wako.