13 Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
14 BWANA huwategemeza wote waangukao,Huwainua wote walioinama chini.
15 Macho ya watu wote yakuelekea Wewe,Nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16 Waufumbua mkono wako,Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
17 BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote,Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
18 BWANA yu karibu na wote wamwitao,Wote wamwitao kwa uaminifu.
19 Atawafanyia wamchao matakwa yao,Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.