17 BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote,Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
18 BWANA yu karibu na wote wamwitao,Wote wamwitao kwa uaminifu.
19 Atawafanyia wamchao matakwa yao,Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
20 BWANA huwahifadhi wote wampendao,Na wote wasio haki atawaangamiza.