2 Kila siku nitakuhimidi,Nitalisifu jina lako milele na milele.
3 BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,Wala ukuu wake hautambulikani.
4 Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako,Kitayatangaza matendo yako makuu.
5 Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako,Na matendo yako yote ya ajabu.
6 Watu watayataja matendo yako ya kutisha,Nami nitausimulia ukuu wako.
7 Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu.Wataiimba haki yako.
8 BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma,Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,