7 Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu.Wataiimba haki yako.
8 BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma,Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
9 BWANA ni mwema kwa watu wote,Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
10 Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru,Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
11 Wataunena utukufu wa ufalme wako,Na kuuhadithia uweza wako.
12 Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13 Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.