1 Haleluya.Ee nafsi yangu, umsifu BWANA.
2 Nitamsifu BWANA muda ninaoishi,Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.
3 Msiwatumainie wakuu,Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake,Siku hiyo mawazo yake yapotea.
5 Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,
6 Aliyezifanya mbingu na nchi,Bahari na vitu vyote vilivyomo.Huishika kweli milele,
7 Huwafanyia hukumu walioonewa,Huwapa wenye njaa chakula;BWANA hufungua waliofungwa;