3 Msiwatumainie wakuu,Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake,Siku hiyo mawazo yake yapotea.
5 Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,
6 Aliyezifanya mbingu na nchi,Bahari na vitu vyote vilivyomo.Huishika kweli milele,
7 Huwafanyia hukumu walioonewa,Huwapa wenye njaa chakula;BWANA hufungua waliofungwa;
8 BWANA huwafumbua macho waliopofuka;BWANA huwainua walioinama;BWANA huwapenda wenye haki;
9 BWANA huwahifadhi wageni;Huwategemeza yatima na mjane;Bali njia ya wasio haki huipotosha.