10 Hapendezwi na nguvu za farasi,Wala hairidhii miguu ya mtu.
11 BWANA huwaridhia wao wamchao,Na kuzitarajia fadhili zake.
12 Msifu BWANA, Ee Yerusalemu;Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
13 Maana ameyakaza mapingo ya malango yako,Amewabariki wanao ndani yako.
14 Ndiye afanyaye amani mipakani mwako,Akushibishaye kwa unono wa ngano.
15 Huipeleka amri yake juu ya nchi,Neno lake lapiga mbio sana.
16 Ndiye atoaye theluji kama sufu,Huimwaga barafu yake kama majivu,