15 Huipeleka amri yake juu ya nchi,Neno lake lapiga mbio sana.
16 Ndiye atoaye theluji kama sufu,Huimwaga barafu yake kama majivu,
17 Hutupa mvua ya mawe kama makombo,Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama?
18 Hulituma neno lake na kuviyeyusha,Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka.
19 Humhubiri Yakobo neno lake,Na Israeli amri zake na hukumu zake.