2 BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu,Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli.
3 Huwaponya waliopondeka moyo,Na kuziganga jeraha zao.
4 Huihesabu idadi ya nyota,Huzipa zote majina.
5 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu,Akili zake hazina mpaka.
6 BWANA huwategemeza wenye upole,Huwaangusha chini wenye jeuri.
7 Mwimbieni BWANA kwa kushukuru,Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi.
8 Huzifunika mbingu kwa mawingu,Huitengenezea nchi mvua,Na kuyameesha majani milimani.